MWANARIADHA Usain Bolt ametania kwa kusema kuwa anasubiri kuitwa kujiunga na kikosi cha Manchester United chini ya Kocha Jose Mourinho.
Bolt raia wa Jamaica ni shabiki mkubwa wa Man United, na amemtabiria Mourinho kuwa atafanya vizuri katika msimu huu akiwa kama kocha wa timu hiyo.
“Bado sijapigiwa simu yoyote lakini naamini nitapigiwa simu ya kujiungana Man United labda inasubiri baada ya kupita kwa Olimpiki,” alitania Bolt ambaye mara kadhaa amekuwa akitembelea Man United.

“Nina furaha kubwa, Mourinho ni chaguo sahihi. Mourinho ni mshindi, anafanya kazi kwa kujituma ili atwae mataji. Sasa anajenga kikosi tungoje kuona kitakachotokea.”
Bolt yupo katika kikosi cha Jamaica kitakachoshiriki Michezo ya Olimpiki mwaka huu huko Brazil akitetea medali ya dhahabu katika mbio za mita 100 na 200.


Post a Comment

 
Top