KUTOKANA na beki wa Azam FC, Shomari Kapombe kuonekana amenenepa kiasi cha kupata kitambi, mchezaji huyo ameanza mazoezi maalum ya kumuweka fiti na kuondoa kitambi hicho.

Kapombe ambaye msimu uliopita alikuwa ndiye beki pekee aliyefunga mabao nane kwenye Ligi Kuu Bara, hakumalizia msimu kutokana na kupatwa na tatizo la kuganda kwa damu na kusababisha akae nje kwa muda wa miezi mitatu.

 Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba, amefunguka kuwa Kapombe yupo chini ya uangalizi wa daktari na kocha ambapo anapewa mazoezi maalumu ya kuhakikisha anarudisha kiwango chake kisha kuanza mazoezi ya pamoja na wachezaji wenzake.

“Hali iliyomtokea Kapombe kwa sasa ni kutokana na kukaa nje kwa muda mrefu bila ya kufanya mazoezi, alianza mazoezi tangu Julai 16,” alisema Kawemba.

Post a Comment

 
Top