MANYIKA JR
PAMOJA na Simba kukamilisha idadi ya makipa watatu, Kocha Joseph Omog ameuambia uongozi usajili kipa mwingine mzoefu.
Omog raia wa Cameroon amewaambia viongozi wa Simba kuwa anahitaji kipa mmoja mzoefu kama ilivyo kwa Vicent Angban.
Habari za uhakika kutoka Simba zinasema, Omog anaamini, Peter Manyika na Denis Richard ambaye amesajiliwa hivi karibuni, bado ni makinda.
“Omog anaona ni bora kuwa na kipa mmoja tu chipukizi na wawili lazima wawe ni wale wenye uwezo unaokaribiana sana.
“Kitengo cha makipa ni muhimu sana, amesisitiza kinapaswa kuwa imara sana ili kuimarisha safu ya ulinzi,” kilieleza chanzo.
Maana yake, kama Simba itasajili kipa mmoja tena, basi Manyika au Denis ambaye alikuwa kwa mkopo Geita Gold Mine na kurudishwa, mmoja wao atalazimika kupunguzwa.

Baada ya suala hilo, uongozi wa Simba unaonekana kuanza kuhaha kwa kuwa wakati ukianza  usajili uliamini suala la kipa limeishapatiwa ufumbuzi.

Uamuzi wa Omog unailazimisha kamati ya usajili ya Simba kurejea tena kuanza kusaka kipa mpya ambaye kocha huyo ataridhika naye.

Post a Comment

 
Top