MSANII wa muziki wa Hip Hop Bongo, Chid Benz amezitaja nyimbo za wasanii wenzake wa Kibongo ambazo anazikubali.
Kupitia Kipindi cha The Playlist cha Times Fm chini ya mtangazaji, Lil Ommy, Chid Benz ambaye kwa sasa anapigana kurejea kwenye gemu kama zamani alisema ngoma anazozikubali ni; 

Piga Makofi ya Professor Jay, Famous ya Juma Mchopanga "Jay Moe", Hao ya Mwasiti, Yote Maisha ya Madee na Mboga Saba ya Mr Blue huku akiitaja Ngoma ya Dar es Salaam Stand Up kama ndiyo wimbo wake bora zaidi aliowahi kufanya.

Post a Comment

 
Top