Mwanafunzi mmoja wa chuo kikuu
kimoja nchini Kenya amejitia kitanzi baada ya kupoteza dau la shilingi 80,000
sawa na dola $800 aliloweka katika mechi za Euro 2016.
Kwa mujibu wa gazeti moja nchini
Daily Nation mwanafunzi huyo alikuwa ameweka dau la dola $ 400 kwa ushindi wa
Ujerumani na pesa zingine sawa na hizo kwa ushindi wa Italia.
Hata hivyo kinyume na matarajio
yake mechi hiyo iliishia sare na kumaanisha kuwa alikuwa amepoteza pesa hizo
zote.
Alifunga safari kutoka mjini
Nairobi hadi kwao magharibi mwa Kenya alipojitia kitanzi nyuma ya nyumba ya
mamake mzazi katika kijiji cha Ondome Uriri jimbo la Nyanza.
Afisa mkuu wa polisi katika eneo
hilo David Kirui anasema kuwa marehemu aliacha ujumbe akisema hakuona haja ya
kuendelea kuishi baada ya kupoteza pesa alizopewa za kulipia karo za chuo
kikuu.
Ujerumani hata hivyo ilishinda
kwa mikwaju ya penalti ilyofuatia.
Ujerumani itachuana dhidi ya
wenyeji Ufaransa katika nusu fainali baadaye leo.
Mshindi kati yao atachuana dhidi
ya Ureno iliyoizaba Wales mabao 2-0 katika mechi ya nusu fainali iliyochezwa
jana.
Sasa miapango ya mazishi imeanza
huku swala la kuenea kwa michezo ya bahati na sibu ikizua tena mjadala miongoni
mwa wapenzi wa kandanda na jamii kwa jumla.
Je kuna njia yeyote ambayo serikali
inaweza kuingilia kati ilikuzuia uraibu wa michezo hiyo ya bahati na sibu
kugeuka na kuwa karaha ?
Post a Comment