Bilionea kijana, Mohammed Dewji
amesema angependa kuwekeza Simba ili kubadili mfumo.
Dewji maarufu kama amewaambia
waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika leo jijini DAr es Salaam kwamba
bajeti ya Yanga na ile ya Azam FC ni mara mbili ya ile ya Simba, jambo
linaloifanya klabu hiyo kuendelea kubaki kuwa msindikizaji.
Tayari Mo amesema yuko tayari kutoa
Sh bilioni 20 ili kununua hisa asilimia 51 na kuwekeza ndani ya Simba.
"Kama unataka mafanikio kwenye
mpira, hakuna zaidi ya fedha. Simba haiwezi kuwa na miaka 80 leo haina hata
uwanja wa mazoezi.
"Unajua kama nikiwekeza fedha
hizo, tunaweza kuzipeleka kwenye mkopo na kuikopesha serikali. Baada ya hapo
tutapata faida ya dola bilioni 7.5 ambazo tutaziingiza kwenye maendeleo.
"Mimi ninaamini Simba haiwezi
kubadilika kwa kuwekeza kwenye bajeti ya Sh milioni 500 kwa mwaka.
Haitawezekana, ndiyo maana nimekuwa nikisisitiza, kwanza Simba inahitaji
muwekezaji na si mdhamini.
"Nisisitize hili,mimi ni
mwanachama wa Simba, ninaumia kuona timu hii inakwenda hivi. Ndiyo maana
ninaingia nikiamini nitaweza kubadilisha mambo kwa kushirikiana na wanachama wa
Simba ili kuleta mabadiliko katika klabu yetu."
Post a Comment