Pop staa Justin Bieber amekata kupokea dola milioni tano za mwanasiasa Donald Trump anayegombea urais kupitia chama cha Republican.

Kwa mujibu wa TMZ Justin amepiga chini dola milioni $5 ilikufanya show kwenye shughuli ya chama cha Republican mjini Cleveland.


Za chini ya kapeti zinasema LeBron James na meneja wa Bieber Scooter Braun wamehusika kumshawishi akatae huku meneja wake akisema ataacha kufanya naye kazi kama atafanya show hio. Justin angefanya show ya dakika 45 tu.

Post a Comment

 
Top