BAADA ya
kuwa kambini kwa wiki mbili, Simba chini ya Kocha Joseph Omog, leo Jumamosi
inacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Burkina Faso kwenye Uwanja wa Jamhuri,
Morogoro.
Simba imepanga kucheza mechi tatu za kirafiki dhidi ya
Burkina Fasso na Polisi Morogoro zote za Ligi Daraja la Kwanza. Mechi mbili ni
dhidi ya Burkina Faso na moja dhidi ya Polisi Morogoro.
Ikiwa kambini Morogoro, Simba imeendelea kupokea
wachezaji mbalimbali kwa ajili ya majaribio kabla ya kusajiliwa na tayari
wachezaji wanne wa kigeni wametimuliwa kwa kutofikia viwango.
Mmoja wa viongozi wa Burkina Fasso, Franky Julius
anayeratibu mechi hizo, alithibitisha kucheza michezo miwili ya kirafiki
kuanzia na ule wa leo Jumamosi.
Julius alisema, baada ya mechi hiyo, Simba itacheza
mchezo mwingine wa kirafiki uwanjani hapo kesho Jumapili dhidi ya Polisi
Morogoro.
Alisema Burkina Faso itacheza mchezo mwingine wa mwisho
wa kirafiki na Simba huko Kilosa, Morogoro wiki ijayo.
“Kama kiongozi wa Burkina Fasso na mratibu wa mechi
zote, tumepanga kucheza mchezo wa kirafiki na Simba kesho (leo), halafu
Jumapili (kesho) Simba watacheza mechi nyingine na Polisi Morogoro kabla ya
kucheza mchezo mwingine wa kirafiki wiki ijayo,” alisema Julius.
Meneja wa Simba, Abbas Ally, alithibitisha uwepo wa
mechi hiyo ya Simba leo kwa kusema: “Jana (juzi Alhamisi) hatukucheza mechi
yoyote ya kirafiki tofauti na watu walivyokuwa wanavumisha, kiukweli
tunatarajia kucheza michezo miwili ya kirafiki baada ya kufanya mazoezi kwa
muda mrefu na lengo ni kocha kuona uwezo wa kila mmoja.”
Post a Comment