KUHUSU tetesi za klabu yake kumuwania mshambuliaji Kipre Tchetche wa Azam FC ambaye inaelezwa kuwa anaondoka klabuni hapo, Rais wa Simba, Evans Aveva alisema hakuna mpango kama huo.

“Nikuhakikishie tu, Simba haikuwahi kuwa kwenye mipango ya kumsajili Tchetche na hizo ni tetesi tu zinazoendelea, kama unavyojua kipindi hiki uvumi ni mwingi.

“Sisi tupo kwenye usajili hivi sasa tunaoendelea kuufanya chini ya kocha wetu, Omog tuliyempa jukumu hilo la kusimamia usajili na tayari wapo wachezaji wa kimataifa na wazawa ambao wamo kwenye mipango yetu kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili.

“Kwa kifupi tumepanga kurejesha heshima yetu iliyopotea kwa kuanza tunaanza na kuuchukua ubingwa wa ligi kuu msimu ujao, hivyo nitahakikisha uongozi wangu uliopo madarakani unafanikisha hilo, kwani tuna kila sababu ya kuuchukua ubingwa huo kwa maana ya kuwa na benchi zuri la ufundi, pia ubora wa wachezaji tuliowasajili,” alisema Aveva.

Post a Comment

 
Top