KOCHA Mkuu wa
Mwadui FC ya mkoani Shinyanga, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, amefunguka kuwawachezaji
wa kimataifa wanaokuja kucheza soka nchini, wengi wao ni waganga njaa kutokana
na kutokuwa na uwezo wa juu kisoka.
Julio ambaye
msimu uliopita alimaliza ligi timu yake ikiwa katika nafasi ya sita kwenye Ligi
Kuu Bara, ameeleza kuwa, hana pupa na usajili kwa kuwa hahofii usajili wa timu
kubwa na badala yake anafanya mambo kwa mahesabu ili kuweza kupata wachezaji
wenye viwango.
Akizungumza,
Julio ameeleza kuwa, hana mpango wa kuleta wachezaji wa kigeni katika kikosi
chake kutokana na kutambua kuwa wengi wao wapo kimaslahi zaidi na wanakuja
kuganga njaa Bongo huku vipaji vyao vikiwa ni vya kawaida.
“Mimi nina
mpango wa kupunguza kikosi msimu huu ambapo msimu uliopita nilisajili wachezaji
33 lakini kwa sasa nitasajili wachezaji 23 kati ya hao, makipa watatu na wachezaji
wa ndani 20.
“Sina haja ya
kusajili maprofesheno kwani asilimia kubwa wapo hapa kwa ajili ya kuganga njaa
tu, hawana kiwango chochote. Wachezaji ambao ni maprofesheno ambao wapo vizuri
wanaocheza ligi kuu ni Ngoma (Donald), Tchetche (Kipre) na Wawa (Pascal)
waliobakia wote hakuna kitu, wanaganga njaa tu,” alisema Julio.
Post a Comment