Multichoice
Tanzania imeonyesha namna ambavyo jamii inaweza kukumbukwa baada ya kutoa
misaada kwa watoto yatima wa kituo cha Al Madina cha Tandale jijini Dar es
Salaam, jana.
Timu nzima ya
Multichoice Tanzania, ilitua katika kituo hicho ikiongozwa na Meneja Mtendaji,
Maharage Chande na kupokewa na watoto hayo walioonekana kuufurahia ugeni huo.
Chande alisema
kuanzia mwaka 2006 wamekuwa wakiwasaidia na wataendelea kuwa nao karibu.
“Februari mwaka
huu, mkuu wa kituo hiki alileta mapendekezo yake kwetu. Sisi tumeamua
kuyafanyia kazi siku chache kabla ya sikukuu,” alisema Chande.
Naye mlezi wa
kituo hicho, Kuluthumu Yusuf alisema: "Nawashukuru sana Dstv kwa kuendelea
kutusaidia, kutoa ni moyo na wanauonyesha kwetu. Tunaomba na makampuni mengine
yaige mfano wao."
Kati ya zawadi
zilizotolewa ni pamoja na mashuka, charahani, magodoro, sukari, mchele na vitu
vingine mbalimbali kwa ajili ya watoto hao.
Multichoice
kupitia DSTv wamekuwa wakionyesha chaneli mbalimbali ambazo ni maarufu nchini
na Afrika nzima kama SuperSport upande wa michezo, M net, Movie Magic na
nyingine upande wa filamu lakini kuna zile maarufu za taarifa ya habari kama
CNN, Al Jazeera, BBC na nyingine nyingi zinazohusisha elimu na burudani.
Post a Comment