Nchini Rwanda kwenye uwanja wa Amahoro jijini
Kigali leo kulikua na pambano la fainali ya kombe la Amani kati ya watani wa
jadi wa Rwanda timu ya jeshi APR na RAYON SPORTS.
Pambano hilo limemalizika kwa RAYON SPORTS kufuta
uteja wa kufunwa mara kwa mara na APR baada ya kuifunga timu hiyo ya jeshi la
ulinzi la Rwanda bao 1 kwa bila mbela ya maelfu ya mashabiki walikua wamefurika
kwenye uwanja huo.
Mchezaji Ismaila Diara kutoka Mali ndiye
aliyefunga goli hilo katika dakika ya 3 kati ya zile 4 za nyongeza baada ya
dakika 90 kutimia.
Mara ya mwisho kwa RAYON SPORTS kuifunga APR
kwenye mchezo wa fainali wa kombe la Amani ilikua ni mwaka 2010 pale mchezaji
marehemu Patrick Mutesa Mafisango alipofunga bao pekee kabla ya kuhamia klabu
ya Simba ya Tanzania.
Kufuatia ushindi huo, RAYON SPORTS wamekabidhiwa
kombe lao mbele ya mke wa rais wa Rwanda Janeth Kagame na maafisa wa shirikisho
la soka la nchi hiyo FERWAFA na wataiwakilisha nchi kwenye michuano ya kombe la
Shirikisho Barani Afrika mwakani.
Post a Comment