![]() |
Chris Smalling akipatiwa matibabu kisiwa cha Bali nchini Indonesia baada ya kuumia PICHA ZAIDI GONGA HAPA
|
BEKI wa
Manchester United, Chris Smalling ameshonwa nyuzi tatu juu ya jicho lake la
kulia baada ya kuumia akiwa mapumzikoni mjini Bali.
Majanga hayo
yamemkuta beki huyo tegemeo wa Mashetani Wekundu akiwa mapumzikoni na mpenzi
wake, Sam Cooke kisiwa hicho cha Indonesia na kukimbizwa hospitali.
Taarifa ya United
imesema Smalling alipoteza fahamu na kuangukia kichwa, baada ya kula chakula
chenye sumu na picha zinamuonyesha mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 akiwa
amefungwa bandeji kichwani, shingoni na mkono wa kushoto.
Tayari Smalling
ameruhusiwa na Madaktari kuondoka hospitali na amerejea kuendelea na mapumziko
yake na atawasili Carrington baadaye mwezi huu kama ilivyopangwa.
Yupo kwenye
mapumziko ya wiki tatu baada ya England kutolewa Euro 2016 Ufaransa na
anatarajiwa kuungana na kikois cha Jose Mourinho kwa ziara ya China kujiandaa
na msimu mpya.
Post a Comment