Uongozi
wa Klabu ya Yanga umesema bado upo katika harakati za kuhakikisha
unamnasa beki wa kushoto wa Simba, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ kwa kuwa
ndiyo chaguo lao.
Tshabalala
ambaye msimu ujao atatambulika kama Zimbwe Jr, alitua Simba kwa mkataba
wa miaka miwili akitokea Kagera Sugar ambapo kwa sasa amekuwa lulu
ndani ya timu hiyo kutokana na kuonyesha uwezo mkubwa.
Mmoja
wa mabosi wa Yanga amesema kuwa wapo katika harakati za kuhakikisha
wanamnasa beki huyo kwa ajili ya kuleta changamoto kwa Mwinyi Haji na
Oscar Joshua kutokana na viwango vyao kuonekana kupwaya.
Bosi
huyo alisema kwa upande wao nafasi iliyobaki katika usajili wa msimu
huu ni beki wa kushoto na kiungo mmoja ambao wataweza kuwasaidia katika
ligi na mashindano ya kimataifa.
“Tunataka
beki wa kushoto na chaguo letu ni Tshabalala wa Simba, huyo ndiyo
atakuwa mtu sahihi wa kuweza kutoa changamoto kwa (Oscar) Joshua na
(Haji) Mwinyi.
“Unajua
tatizo halipo kwa mchezaji kwa sababu tumeshakutana naye zaidi ya mara
nne na ameonyesha kukubali isipokuwa Simba ndiyo wanaonekana kuwa ni
wagumu kwa kuwa bado wanamkataba naye wa mwaka mmoja,” alisema bosi
huyo.
Alipotafutwa
Ofisa Habari wa Yanga, Jerry Murro alisema kuwa kwa sasa hawezi
kuliongelea suala hilo kwa kuwa bado halijafika mezani kwake.
Ikumbukwe
kuwa, hivi karibuni uongozi wa Simba uliwahi kusema hauna mpango wa
kumuuza mchezaji huyo kutokana na kuwa ni msaada mkubwa ndani ya timu
hiyo.
SOURCE: CHAMPIONI
Post a Comment