Kocha
Mganda, Jackson Mayanja aliyeelezwa kuwa mbioni kuachana na Simba
kutokana na sababu mbalimbali, ametua jijini Dar, juzi usiku na
kufunguka kuhusiana na kocha mkuu mpya wa timu hiyo, Joseph Omog.
Mayanja
ambaye ametua nchini akitokea Uganda alikokwenda kwa ajili ya mapumziko
mara baada ya kumalizika kwa ligi msimu uliopita, hivi karibuni
kuliibuka taarifa zilizodai kuwa hayupo tayari kufanya kazi chini ya
Omog lakini amekanusha hilo.
“Kama
nikielewana na Simba nitafanya kazi tu chini ya Omog kwa kuwa nafahamu
majukumu yangu kama kocha msaidizi,” alisema Mayanja.
Omog |
Awali
kulikuwa na taarifa kuwa Mayanja anaweza kutua katika timu yake ya
zamani ya Kagera Sugar au Mwadui FC, ambapo yeye mwenyewe amekiri
kufanya mazungumzo na klabu hizo kwa kuwa mkataba wake na Simba
ulimalizika.
“Kweli
Kagera na Mwadui wananihitaji, hata Kiyovu SC ya Rwanda pia lakini nipo
Dar kwa kuwa nimetumiwa tiketi na Simba. Hivyo, nitawasikiliza Simba
kwanza baada ya hapo ndiyo kitakachofuata,” alisema kocha huyo.
Taarifa za ndani ya Simba zinaeleza kuwa Mayanja alitarajiwa kukutana na Omog, jana kwa ajili ya mazungumzo.
Akiwa
kocha wa muda wa Simba, Mayanja aliiongoza Simba katika mechi 16 za
Ligi Kuu Bara na kushinda 11, sare moja na kupoteza nne dhidi ya Yanga,
Mwadui, Toto African na JKT Ruvu.
SOURCE: CHAMPIONI
Post a Comment