KIUNGO Mshambuliaji wa zamani wa Simba, ambaye sasa anacheza soka la kulipwa nchini Afrika Kusini katika Klabu ya Royal Eagles iliyopo Ligi Daraja la Kwanza nchini humo amesema alikuja kucheza ndondo ili aonyeshe kiwango chake na pia aitwe timu ya taifa.
Akizunguma kutoka Afrika Kusini, Uhuru alisema: “Nilicheza Ndondo Cup sio kwa kutaka pesa au lah ... ila ni kuwaonesha Watanzania uwezo wangu ulivyo kwa sasa hasa ukija katika suala la ufungaji magoli. Nilishiriki pia Michuano ya Ramdhani Cup na nikaibuka mfungaji bora nikiwa na magoli saba katika mechi tano.
Katika Michuano ya Ndondo Cup, Uhuru alikuwa akiitumikia Temeke Market.

Post a Comment

 
Top