SIMBA SC
inatarajiwa kuondoka mjini Dar es Salaam keshokutwa kwenda Morogoro kuweka
kambi ya kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, ambao
utanatarajiwa kuanza kuanzia Agosti 20, mwaka huu.
Na baada ya
maandalizi mazuri ya takriban mwezi mzima, Simba imeialika klabu bingwa ya
Kenya, Gor Mahia kwa ajili ya kuja nchini kucheza mechi ya kirafiki katika
Tamasha la Simba Day, Agosti 8.
Akizungumza jana,
Rais wa Simba, Evans Elieza Aveva alisema kwamba uongozi wa timu hiyo uliamua
kuahirisha programu ya mazoezi iliyopangwa kuanza jana mjini Dar es Salaam kwa
ajili ya kupisha sherehe za Sikukuu ya Eid El Fitri.
Meneja huyo
wa zamani wa Embassy Hotel, Aveva alisema kuwa wachezaji wote waliosajiliwa na
timu hiyo watakwenda kambini Morogoro kwa ajili ya kuanza kujifua wakiwa chini
ya Kocha Mkuu mpya Mcameroon Joseph Marius Omog ambaye aliwasili nchini wiki
iliyopita na kurithi mikoba ya Muingereza Dylan Kerr, aliyefukuzwa Januari.
"Kila
kitu kinakwenda vizuri na Mungu akijaalia baada ya sikukuu kupita, timu
itakwenda Morogoro na si Lushoto kama ilivyoandikwa na gazeti moja,"
alisema Aveva.
Post a Comment