CRISTIANO
RONALDO na wenzake wa Ureno jana wamewasili nyumbani
katika Jiji la Lisbon baada ya kuushtua ulimwengu kwa kutwaa taji la
Euro 2016.
Taji hilo
halikuwa mbali ya mikono ya nahodha
Ronaldo, ambaye pamoja na kikosi kizima kilipewa mapokezi makubwa baada ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Humberto Delgado.
Mara baada
ya kutua, ndege yao ilipokelewa kwa
kurushwa maji yenye rangi nyekundu na kijani juu ya ndege hiyo.
Kwa ushindi
huo ambao haukutarajiwa ulilazimisha kujengwa kwa uzio mzito katika mapokezi hayo ya Lisbon, ambapo maelfu
ya mashabiki walifurika mitaani, wakicheza, wakiimba na kupunga mikono wakiwa
na bendera za Ureno zenye rangi nyekundu na kijani.
Sherehe
ziliendelea Jumatatu, na Ronaldo na wenzake walitua katika uwanja huo wa ndege saa 5:15 na kwenda kumuona Rais, Marcelo Rebelo de Sousa katika
makazi yake ya serikali kabla ya gwaride kuingia katika mitaa ya Lisbon.
Na Rais
alisema : " Sisi ndio bora Ulaya. Tumeonyesha kile tulichokifanya: nguvu,
umoja, tumeweza kushinda mambo yote magumu ikiwemo kuumizwa na kumkosa
Cristiano Ronaldo."
Ndoto za
Ureno kulibeba taji hilo ziliingia katika wasiwasi mkubwa baada ya Ronaldo kuumizwa, nahodha na hirizi
hiyo ya Ureno, alianguka uwanjani katika dakika ya nane kufuatia kuumizwa na Dimitri Payet.
Baada ya
kutibiwa mara mbili na kujaribu kurudi uwanjani, Ronaldo alishindwa kuendelea
na mchezo na kutolewa.
Ufaransa iliendelea kutawala mchezo dhidi ya
Ureno na pongezi ziende kwa mchezaji bora wa mechi, beki Pepe na kipa Rui
Patricio aliyeokoa hatari kadhaa.
Katika hatua
nyingine, Ronaldo alisema: " Haikuwa fainali niliyoitaka lakini nina furaha kubwa. Ni Kombe la Wareno
wote, kwa wahamiaji wote, kwa watu wote waliotuamini, kwa hiyo nina furaha na ninajivunia."
Post a Comment