NAHODHA wa timu ya Taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo ameamua kumpa kiungo Luis Nani kiatu cha Silva alichopewa kama zawadi baada ya kufunga mabao matatu na kusaidia upatikanaji wa mabao mengine mawili kwenye Michuano ya EURO 2016 iliyomalizika kwa timu hiyo ya taifa kutwaa ubingwa baada ya kuwafunga wenyeji Ufaransa bao 1-0.

Kiatu cha dhahabu, kilinyakuliwa na Antoine Griezmann aliyefanikiwa kufunga mabao sita na kusaidia upatikanaji wa mengine mawili.
Baada ya kukabidhiwa kiatu hicho,  Nani aliyechangia kwa kiasi kikubwa kupatikana kwa ubingwa huo aliandika kwenye ukurasa wake wa Mtandao wa Kijamii wa Instagram maneno ya kumshukuru Ronaldo huku akimtaja kuwa zaidi ya nahodha na ni bingwa wa ukweli.

Post a Comment

 
Top