Mbunge wa Mikumi
na msanii mkongwe wa muziki wa Hip Hop Bongo, Joseph Haule maarufu kama
Professor Jay amesema mafanikio kwa msanii siyo kumiliki mali nyingi bali ni
jamii kuweza kunufaika kutokana na kipaji chake
Akiongea na Dj
Niko Track kwenye kipindi cha Dj Show cha Radio One, Professor Jay alisema kuwa
mafanikio ni kitu kile kinachoonekana na kuleta tija na maendeleao kwa watu,
lakini pia yanaweza kugawanyika kwa watu wengine siyo ya kwako peke yako.
“Wasanii
waliofanikiwa majina yao yanaweza yakatumika kama alama ili kuinufaisha jamii.
Wasanii kama Lady Jaydee, Professor, Juma Nature ni wasanii ambao kwa talent
zao walizokuwa nazo zimekuwa manufaa kwa wengine. Kama Lady Jaydee amekuwa icon
kwa wakina mama ambao wamekuwa strong kuweza kusimama pale. Mafanikio siyo kuwa
na nyumba wala gari hapana, talent yangu imesaidia nini jamii yangu,” alisema
Professor.
Kama Professa
unakuta ana ‘Professor Foundation’ ambayo inasaidia hata wasiokuwa wanamuziki
wananufaika kwa kidogo ninachokirudisha kwenye jamii. Wale wote wenye mafanikio
ni wale wanaoweza kushare na kuruidisha kidogo walichokuwa nacho kwenye jamii,”
aliongeza.
Post a Comment