BAADA
ya kikosi cha timu ya Medeama kuwasili nchini kikitokea Ghana, kocha mkuu wa
kikosi hicho, Prince Yaw Owusu, amefunguka kuwa anawajua vizuri wapinzani wake,
Yanga, hivyo ana uhakika wa ushindi.
Medeama
ilitua jana mchana kwa ajili ya mchezo wao wa kesho Jumamosi dhidi ya Yanga wa Kombe
la Shirikisho Afrika unaotarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.
Msafara
wa Medeama una watu 32 ambao ni wachezaji 19, viongozi wa benchi la ufundi
sita, waandishi wa habari wawili na viongozi wengine watano.
Akizungumza
muda mfupi baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere, Owusu alisema hii si mara yake ya kwanza kuja Tanzania kwa kuwa miezi
michache iliyopita alikuja na kikosi cha Al Khartoum cha Sudan kwenye michuano
ya Kombe la Kagame.
“Naijua
Yanga vizuri tu kwani miezi michache iliyopita nilikuwa hapa na kikosi cha Al
Khartoum kwenye Kagame nikiwa kocha msaidizi huku kocha mkuu akiwa ni Kwesi
Appiah.
“Lakini
kwa wachezaji wangu wote hii ni mara yao ya kwanza kuja hapa, lakini
tumejiandaa kwa mapambano ili kuondoka na pointi zote tatu ambazo ndizo
tunazihitaji kufikia malengo yetu ya hapo baadaye kucheza nusu fainali,”
alisema Owusu.
Naye
nahodha wa kikosi hicho, Mohammed Muntari Tagoe ambaye ni kipa alisema wamekuja
kushindana na wale wanaowabeza basi wasubiri kuona kitakachotokea uwanjani.
Post a Comment