Masau Bwire kushoto

YANGA nafasi ya kusonga mbele bado ipo, msife moyo wala kukata tamaa! Askari vitani akizidiwa anarudi nyuma, si kukimbia kwa kuogopa kufa bali kujipanga kwa mashambulizi ya ushindi!
Jipangeni kwa mashambulizi ya ushindi katika mechi zilizosalia. Najua ni ngumu lakini tukitia nia inawezekana!
Lakini washabiki na sisi, khaa, tunaboa! Tunashindwa kweli kushangilia mpaka mwisho wa mchezo!
Jana Medeama wakiwa nyuma bao moja walianza mashambulizi na kuonekana kuielemea timu yetu, hali hiyo ikawanyamazisha kabisa washabiki wetu!
Hiyo iliongeza nguvu kwa Medeama na kushusha morari kwa wachezaji wetu kwani, miongoni mwetu tulianza kuwasema vibaya baadhi ya wachezaji wetu! Hiyo ni mbaya, tuiache!

Yanga mbele........

Post a Comment

 
Top