MSHAMBULIAJI anayewaniwa na Simba SC,
Mrundi Laudit Mavugo inadaiwa ametimkia Ufaransa kufanya mipango ya kujiunga na
klabu ya Tours ya Ligi Daraja la Pili, maarufu kama Ligue 2.
Na Mavugo anakwenda Ufaransa wakati
tayari Simba SC wamesema wamekwishaingia Mkataba na mchezaji huyo kuanza
kuwatumikia kuanzia msimu ujao.
Wakala Dennis Kadito aliyewahi
kumsimamia wakati fulani mchezaji huyo apate timu Ulaya amesema kwamba amesikia
taarifa za Mavugo kwenda Ufaransa, lakini hahusiki na hajui lolote.
"Nimesikia tu, kwa nini
msimuulize yeye mwenyewe,"alisema Kadito ambaye mwaka jana alijaribu
kumleta Simba SC mchezaji huyo.
Lakini mchezaji mwenzake Mavugo katika
timu ya taifa ya Burundi ametihibitishia leo kwamba mwana Int'hamba Murugamba
mwenzake huyo amekwenda Ufaransa.
Alisema siku Mavugo anaondoka
alikutana naye Uwanja wa Ndege wa Bujumbura akiwa na familia yake ikimuaga kwa
ajili ya safari ya kuelekea nchini humo.
"Nilikutana naye Uwanja wa Ndege
wa Burundi, akiwa na familia yake wakimuanga, kwani amepata ofa ya kwenda
Ufaransa kufanya majaribio katika timu ya Tours inayoshiriki Ligi Daraja la
Pili," alisema rafiki huyo.
Bado haijulikani Simba SC itachukua
gani kwa Mavugo, kwa kuwa makubaliano yao na mchezaji huyo bado yanafanywa siri
ili kuepuka vikwazo kutoka klabu yake, Vital'O.
CHANZO: BIN ZUBEIRY
Post a Comment