KIUNGO mshambuliaji
wa Simba, Shiza Kichuya amesema kuwa anaamini msimu ujao kikosi hicho kitafanya
maajabu.
Kikosi cha Simba kipo mkoani Morogoro
kikiendelea kujifua kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa
kuanza kutimua vumbi Agosti, mwaka huu.
Akizungumza kutoka Morogoro, Kichuya ambaye
amesajiliwa akitokea Mtibwa Sugar, amesema kikosi chao ni bora na kitafanya
mambo makubwa msimu ujao.
Alisema kwa upande wake ametua Simba kufanya
kazi na siyo Simba imfanyie kazi, hivyo atahakikisha anashirikiana vilivyo na
wenzake pamoja na benchi zima la ufundi.
“Ndoto zangu siku zote ilikuwa ni kucheza
katika moja ya timu kubwa hapa nchini, hilo limetimia, kilichobaki sasa ni mimi
kufanya kazi yangu hapa Simba na sitasubiri inifanyie kazi.
“Nasema hivyo kwa sababu nataka msimu ujao
tufanye mapinduzi makubwa na nitashirikiana na wenzangu kuhakikisha hilo
linatimia,” alisema Kichuya.
Post a Comment