KIUNGO mshambuliaji mpya wa Simba, Shiza Kichuya, amesema amejiandaa vya kutosha ili kuhakikisha anapata namba katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo.

Kichuya aliyetua Simba akitokea Mtibwa Sugar, alisema lengo lake ni kuhakikisha anaingia katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo na kuisaidia kwa kiasi kikubwa katika Ligi Kuu Bara msimu ujao.

Hata hivyo, alikiri kuwa atalazimika kupambana kwa nguvu kutokana na kikosi cha timu hiyo kuwa na wachezaji wazuri na wenye uwezo mkubwa uwanjani.

“Lengo ni kuingia katika kikosi cha kwanza lakini niseme si kazi rahisi, hivyo nitapambana ili niweze kupata nafasi ya kucheza,” alisema Kichuya.

Post a Comment

 
Top