LICHA ya kutoka sare ya bao 1-1 na Medeama, Kocha wa Yanga,
Hans van Der Pluijm amesema ana imani kubwa kikosi chake hicho kitatinga nusu
fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Yanga ambayo ina alama moja baada ya kushuka dimbani mara
tatu, kimahesabu bado ina nafasi kwani ina mechi tatu na kati ya hizo moja
inacheza nyumbani hivyo ikipata ushindi kwenye michezo hiyo inaweza kutinga
hatua inayofuata.
Pluijm alisema vijana wake walipambana katika mchezo wa jana
lakini bahati haikuwa yao kwani walishindwa kuzitumia nafasi walizozipata.
"Ukiniuliza kuwa tunaweza kufuzu katika hatua ya nusu
fainali jibu lake ni ndiyo kwakuwa katika mpira kila kitu
kinawezekana,tumebakiwa na mechi tatu na tukishinda zote tutakuwa na alama
kumi," alisema Hans.
Naye Kocha wa Medeama, Pride Yaw Owusu alisema Yanga
walicheza vizuri lakini wao lengo lao lilikuwa ni kupata pointi moja ambayo
walifanikiwa kuinyakua.
Baada ya matokeo ya jana kundi lao lipo hivi:
CAF Confederation Cup
Group A
P W D L Pts
1 TP Mazembe 2 2 0 0 6
2 Mo Bejaia 2 1 1 0 4
3 Medeama 3 0 2 1 2
4 Yanga 3 0 1 2 1
Post a Comment