TIMU ya Kagera Sugar imepania kufanya vizuri katika msimu ujao baada ya
kuendelea kuimarisha kikosi chake kwa kusajili wachezaji wawili wazoefu na
mikikimikiki ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
Nyota waliomwaga wino kwa ajili ya kuitumikia kagera ni kipa Hussein
Shariffu 'Cassilas' na winga Ibrahim Twaha 'Messi'.
Chanzo kutoka ndani ya klabu hiyo kimekiri kuwavutia nyota hao huku kocha
mpya wa kikosi hicho Mecky Mexime akikiri kwa kusema ni kweli wamewasajili ili
kukiongezea nguvu msimu ujao, ikumbukwe Kagera ilijiokoa kwenye hatari ya kushuka
daraja msimu ulioisha hivyo msimu ujao hawataki kufanya tena makosa hayo.
Nyota hao wote wamewahi kuichezea Simba SC lakini hawakudumu.
Post a Comment