Sasa iko wazi, mahakama ya usuluhishaji wa masuala ya michezo, CAS imepanga Agosti 25, mwaka huu kuwa ndio siku ya kusikiliza rufaa iliyowasilishwa na rais wa zamani wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Sepp Blatter ya kupinga kufungiwa kujihusisha na masuala ya soka kwa muda wa miaka 6.
Sepp Blatter mwenye miaka 80 na rais wa zamani wa Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA), Michel Platini mwaka jana walikutwa na hatia ya kuvunja maadili ya kwa kuvuja paundi milioni 1 .3.
Platini alilazimika kujiuzulu mwezi wa 5 mwaka huu ndani ya bodi hiyo ya soka Ulaya baada ya kuungiwa miaka 6 kutokujishughulisha na masuala ya michezo. Hata hivyo viongozi wote hao wawili wanapingwa kushiriki kwenye soka la aina yoyote.

Post a Comment

 
Top