Mkali
wa Hip Hop Bongo, Sharif Thabiti Ramadhani ‘Darasa’ amefunguka kuwa anaheshimu
maneno ya msanii mwenzake, Estalina Sanga ‘Linah’ kuwa anamkubali na kutamani
kuwa na mwanaume mwenye sifa kama zake lakini yeye ana mpenzi wake wa muda mrefu.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda alipotembelea
Global TV Online wikiendi iliyopita, Darasa alisema kuwa Linah ametumia ujasiri
kutoa hisia zake na amefurahi kusikia anamkubali ingawa yeye ana mpenzi wake wa
muda mrefu na wanaaminiana.
“Namshukuru kwa kunikubali,
kiukweli namheshimu na nimefurahi,” alisema Darasa.
Darasa alifunguka hayo baada ya
hivi karibuni Linah kueleza hisia zake kwenye mitandao ya kijamii kuwa
anatamani awe na mwanaume mwenye sifa alizonazo Darasa.
Post a Comment