Michuano ya Kombe la dunia 2018 itakayofanyika Urusi
inakaribia kuanza kwani bado mwaka mmoja na miezi kadhaa, kwa kawaida Kombe la
dunia hufanyika kila baada ya miaka minne, hivyo kama una mpango wa kwenda
kuangalia mechi za Kombe la dunia 2018, ninazo bei za tiketi.
Shirikisho la soka ulimwenguni FIFA limeripotiwa na
101goals.com kutaja bei za tiketi za michuano hiyo itakayoanza 2018, bei ya
tiketi ya michuano hiyo itaanzia dola 105 kwa raia wa kigeni ambazo ni zaidi ya
Tsh 230,000, lakini bei ya tiketi za fainali ya michuano hiyo inatajwa kuwa
itafikia dola 1100 ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 2.4.
Kwa watu ambao makazi yao ni Urusi bei ya tiketi hizo kwa
kima cha chini watauziwa dola 20 ambazo ni Tsh 40,000.
Post a Comment