Na Mwandishi Wetu
Biashara ya muziki imekuwa na faida kubwa ukilinganisha na miaka ya nyuma, nimeipata
good news ya wasanii wanaounda kundi la Navy Kenzo (Aika & Nahreel)
kuhusiana na kuanza ujenzi wa nyumba yao yenye thamani ya milioni 700, Ayo TV iliwapata Navy Kenzo
kuzungumzia nyumba hiyo, pamoja na sehemu ya video ya ujenzi ulipofikia.
“Mwaka huu ni mwaka ambao umekuwa wa mafanikio na tumefanya
vitu vingi pamoja na tour na tumepata dili nyingi ambazo zimetuingizia pesa,
ndio tulikuwa na mipango ya kujenga nyumba toka zamani na imefikia wakati
tumeanza kujenga, hii ni nyumba ambayo tumebuni mimi na Aika na itagharimu
milioni 700 hadi kuisha”
Post a Comment