Dar
es Salaam. Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limeufungia rasmi wimbo wa ‘pale
kati patamu’ ulioimbwa na msanii Ney wa Mitego kutokana na ukiukwaji mkubwa wa
maadili.
Taarifa
iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Katibu Mtendaji wa BASATA, Godfrey
Mngereza ameeleza kuwa msanii huyo amekuwa na tabia na mienendo yenye kuchafua
sekta ya sanaa yeye binafsi kupitia kutoa kazi chafu na kufanya maonyesho yenye
kukiuka maadili.
“Kazi
zake zikikiuka maadili na kudhalilisha utu wa mwanamke sambamba na kutoa lugha
za matusi na za kudhalilisha watu wa kada mbalimbali.”
Ameeleza
ieleweke kwamba kwa mujibu wa kifungu namba 4(L) cha Sheria ya BASATA namba 23
ya mwaka 1984, Baraza limepewa jukumu la kuhakikisha linalinda maadili miongoni
mwa wasanii wanapokuwa jukwaani au wanapobuni kazi yoyote ya sanaa.
“Ikumbukwe
kwamba BASATA limeshamuita na kumuonya msanii huyu mara kadhaa kutokana na
tabia yake ya kutoa kazi zisizokuwa na maadili na aliahidi kubadilika na
kuachana na tabia hiyo.
Kwa
hiyo kuendelea kwake kufanya matukio haya kwa makusudi ni uthibitisho kwamba
hajabadilika na kwa maana hiyo ameendelea kuidhalilisha sanaa na wasanii wa
kitanzania wenye kujitambua na kuiheshimu kazi ya sanaa kama kazi nyingine.
Kwa
sasa Msanii huyu ametoa wimbo mwingine wa Pale Kati Patamu ambao uko mitandaoni
ukipambwa na picha chafu zinazoonesha mwanamke akiwa mtupu yaani uchi wa
mnyama.”
CHANZO:
Thechoice
Post a Comment