![]() |
kikosi cha stand united |
MSHAMBULIAJI
wa zamani wa klabu ya Simba Adam Kingwande amejiunga na Stand United ya mkoani
Shinyanga akitokea Kagera Sugar kwa kandarasi ya mwaka mmoja.
Stand
inayodhaminiwa na kampuni ya uchimbaji wa madini ya ACACIA imeanza kujipanga
kwa ajili ya msimu ujao baada ya kuwasainisha wachezaji waliofanya vizuri
katika ligi iliyomalizika. Mbali na Kingwande wachezaji wengine waliosajiliwa
ni Erick Mlilo na Miraji Maka toka Toto African ya Mwanza.
Afisa
Habari wa klabu hiyo Deo Kaji Makomba amesema kuwa usajili huo umezingatia
matakwa ya kocha wao Mfaransa Patrick Liewig kwa kuziba sehemu zenye
mapungufu ndani ya kikosi hicho.
"Ripoti
ya mwalimu ndiyo tunaifanyia kazi, tunaendelea kujipanga kwa ajili ya msimu
ujao na bado tunawaangalia wachezaji wengine wa kuwaongeza," alisema
Makomba.
Wakati
huo huo Stand maarufu kama 'Chama la Wana' wapo katika hatua za mwisho za
kuingia mkataba na kocha msaidizi raia wa Ufaransa Guillaume Denis ambaye atakuwa pamoja na
Athumani Bilali kumsaidia Liewig.
"Mazungumzo
yanaendelea vizuri muda si mrefu tutaingia nae kandarasi kwa ajili ya
kuitumikia timu yetu msimu ujao," alisema Makomba.
BOIPLUS
Post a Comment