MASHABIKI wa Yanga
juzi walipagawa baada ya shuti lililopigwa na kipa wa timu hiyo Deogratius
Munishi ‘Dida’ kuzama ndani ya gari aina ya Toyota Noah.
Yanga kwa sasa inajiandaa na mchezo wake wa
hatua ya makundi katika Kombe la Shrikisho Afrika dhidi ya Medeama ya Ghana,
baada ya kuwa wameshapoteza michezo miwili dhidi ya MO Bejaia na TP Mazembe.
Katika mazoezi ya juzi kwenye Uwanja wa Boko
Veterani, Dida akiwa na makipa wenzake walikuwa wakipigiana mashuti langoni
huku wakisimamiwa na kocha wa makipa, Juma Pondamali.
Hata hivyo, shuti la Dida ndiyo lilizua gumzo
baada ya kupita kwenye kioo cha gari lililokuwa limepaki nje ya uwanja huo na
kwenda siti ya nyuma.
Dida ambaye alionekana kusifiwa kila mara
kutokana na kupiga mashuti makali alipiga mpira huo ambao ulipaa juu ya lango
na kwenda kupenya kwenye kioo cha gari hilo na kuzua gumzo kwani lilikuwa mbali
na uwanja huo.
Hali hiyo iliwafanya baadhi ya mashabiki
kusogea katika gari hilo na kuanza kulitazama.
Shabiki mmoja alisikika akisema: “Dah huyu
Dida kama angekuwa mshambuliaji basi angekuwa anafunga sana, ni vigumu mpira
kupita kwenye hiki kioo ambacho kimefungwa kidogo.”
Post a Comment