KAMATI ya maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imemfungia
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga Jerry Muro mwaka mmoja
kujihusisha na masuala ya soka pamoja na faini ya Sh. Milioni 3.
Kamati hiyo iliyokaa jana Julai 7 chini wa Mwenyekiti Wakili
Wilson Ogunde imemkuta Jerry akiwa na makosa matatu yaliyowasilishwa kwao.
Kosa la kwanza ni kudharau maamuzi ya Kamati ya Nidhamu ya
TFF mwaka 2015 alipotakiwa kulipa faini ya Sh. Milioni 5 baada ya kufanya
makosa ambapo hajaweza kulipa hadi leo.
Kosa la pili ni kuchochea
vurugu na kuhatarisha amani kuelekea mchezo wa Kundi A Kombe la Shirikisho kati
ya Yanga na TP Mazembe ya DR Congo.
Katika shitaka hilo, Jerry aliwahamasisha mashabiki wa timu
hiyo kukaa pande zote hata ule wa watani wao Simba kitu ambacho kingesababisha
uvunjifu wa amani.
Katika shitaka la tatu Muro alifanikiwa kuishinda TFF
katika kupingana na maamuzi ya
shirikisho hilo juu ya masuala ya utoaji wa haki za matangazo ya Televisheni.
Licha ya hukumu hiyo Muro ana haki ya kukata rufaa katika
Kamati ya Rufaa ya TFF.
Post a Comment