WAKATI kambi ya Simba ikizidi kuchanganya huko
mkoani Morogoro, kocha msaidizi wa timu hiyo, Jackson Mayanja, amesema kikosi
chao kitakuwa moto msimu ujao kwani kina wachezaji sahihi kuliko msimu
uliopita.
Kauli
hiyo ya Mayanja raia wa Uganda inakuja wakati kocha mkuu wa timu hiyo, Joseph
Omog akisisitiza zaidi wachezaji kuwa na stamina itakayowawezesha kupambana
dakika zote uwanjani.
Mayanja
amesema, mwanga umeanza kuonekana na anawapongeza viongozi kwa kusajili
wachezaji ambao aliwapendekeza.
“Tutakuwa
moto sana msimu ujao kwa sababu kikosi chetu kimejaa wachezaji walio na viwango
ambao niliwaomba viongozi wawasajili.
“Kikubwa
ambacho tunataka ni tupewe muda tu wa kuingiza ufundi wetu na Simba mbona
itarejea kwenye mstari wake,” alisema Mayanja.
Katika
mazoezi ya Simba kambini Morogoro, Kocha Omog ameonekana kuvalia njuga mazoezi
ya fiziki ili kuwaongezea stamina wachezaji wake.
Post a Comment