CHIRWA WA PILI KUTOKA KULIA WALIOSIMAMA
Mshambuliaji wa Yanga Obey Chirwa natarajia kurejea nchini ndani ya siku chache akitokea kwao Zambia.

Mmoja wa rafiki zake wa karibu, amesema matatizo yaliyompeleka Zambia ameyafanyia kazi na atarejea ndani ya siku chache.

“Hatakaa sana, kila kitu ameshughulikia. Ingawa ni mambo mengi, atalazimika kuacha mengine yashughulikiwe,” kilieleza chanzo.

Chirwa anarejea haraka ili kuendelea na na maandalizi ya mechi ya Kombe la Shirikisho Kundi A dhidi ya Medeama ya Ghana.


Mechi hiyo itapigwa Julai 16 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Post a Comment

 
Top