Isihaka kulia


BEKI na nahodha wa zamani wa Simba, Hassan Isihaka ameripotiwa kusaini mkataba wa miaka mawili na Klabu ya Ndanda FC ya Mtwara.
Isihaka ambaye anamudu kucheza beki ya kati, hakuwa na msimu mzuri 2015/16 hususan kuanzia mzunguko wa pili baada ya Simba kuchukuliwa na kocha Jackson Mayanja aliyebeba mikoba ya Muingreeza Dylan Kerr.
Chanzo kinadai kuwa Isihaka ambaye pia alihusishwa kutolewa kwa mkopo na Simba kwenda Mbao FC ya Mwanza,  amepewa mkataba huo wa miaka mawili na Ndanda ili akakiongezee nguvu kikosi hicho msimu ujao.

Post a Comment

 
Top