Ile sekeseke kati ya klabu ya Yanga
na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuhusiana na suala la mapato, jana
liliendelea na kuzua tafrani kubwa.
Ishu hiyo ilizuka mara baada ya mechi
kati ya Yanga dhidi ya Medeama kwisha kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam.
Baada ya hapo, fedha zilihesabiwa na
lilipofikia suala la mgawo, uongozi wa Yanga ulikubali lakini kwa sharti moja,
kutoa hundi na si fedha taslimu.
Yanga walisema wameamua fedha zote
ziende benki na usiku huo wangezikabidhi kwenye kampuni ya ulinzi, kesho
zingepelekwa benki na baada ya hapo, mgawo ungepitia mfumo wa hundi.
Kwa kuwa hilo halijazoeleka, TFF
iliendelea kusisitiza kwamba watu wapewe mgawo wao "cash cash" kama
ilivyozoeleka, Yanga wakashikilia msimamo wao.
Suala hilo baadaye liliamuliwa na
Serikali na inaelezwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye
alitaka zisigawiwe ili kuwe na utaratibu sahihi.
Hali hiyo ilisitisha malumbano lakini
inaonekana TFF ilikwazika kupita kiasi kutokana na Yanga kuanzisha utaratibu
huo.
Lakini upande wa Yanga, ulijieleza
kwamba umepanga kufanya hivyo ili kutumia mashine za EFD wakati wa malipo na
itatoa lisiti kwa kila watakaolipwa.
Kabla ya mechi ya Medeama, kulikuwa
na tafrani kubwa kati ya TFF na Yanga baada ya klabu hiyo kuruhusu mashabiki
kuingia bure katika mechi ya TP Mazembe.
TFF iliambulia patupu, hali iliyofanya
kuandika barua kadhaa ikidai ilipwe huku ikikadiria idadi ya watu uwanjani,
jambo ambalo halikuwezekana.
CHANZO: Salehjembe
Post a Comment