Raul Gonzalez Blanco


MADRID, Hispania
NYOTA wa zamani wa Real Madrid, Raul Gonzalez Blanco amewatuliza mashabiki wa kikosi hicho kwa kusema, timu yao itaendelea kupata mafanikio hata kama Cristiano Ronaldo ataondoka.
Ronaldo raia wa Ureno amekuwa msaada mkubwa wa Madrid tangu alipojiunga na timu hiyo mwaka 2009 akitokea Manchester United ambapo usajili wake ulivunja rekodi kwani alinunuliwa kwa dau la pauni milioni 80 sawa na Sh bilioni 226.9.

Msimu uliopita, Ronaldo alivunja rekodi ya ufungaji ya Raul kikosini na kuiwezesha timu yake kutwaa ubingwa wa 11 wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.
"Kuna maisha mengine mazuri baada ya Ronaldo," alisema Raul na kuongeza: "Ronaldo amefanya mambo makubwa hapa, lakini Madrid ni timu kubwa yenye wachezaji wakubwa wa kuendeleza mafanikio.
"Ronaldo amekuwa mfungaji bora kwa misimu saba, hakuna aliyefikiri kama itakuwa hivyo, jambo la msingi ni kuendelea kujituma kama timu na hata kama (Ronaldo) akiondoka.”

Post a Comment

 
Top