UONGOZI wa Yanga, umesema kuwa
unawaruhu mchezaji ambaye mkataba umemalizika kuondoka kama ataona maslahi yake
ni madogo kwenye timu hiyo inayojiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara.
Kauli hiyo, ameitoa kutokana na
idadi kubwa ya wachezaji ambao mikataba yao inamalizika mwishoni mwa msimu huu
wa ligi ambao ni Vicent Bossou, Haroun Niyonzima, Donald Ngoma.
Wengine ni Haji Mwinyi, Nadir
Haroub 'Cannavaro', Deus Kaseke, Anthony Matheo, Thabani Kamusoko, Amissi
Tambwe na Mbuyu Twite ambaye yeye mkataba wake umemalizika mwezi huu.
Makamu Mwenyekiti wa timu hiyo,
Clement Sanga alisema bado wanahitaji kuendelea na wachezaji wote kwenye misimu
mingine ijayo ya ligi kuu, lakini hawatamzuia yule atakayetaka kuondoka kufuata
maslahi mazuri.
Sanga alisema, kanuni za
Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), zinawaruhusu wachezaji hao kufanya
mazungumzo na klabu nyingine watakazohitaji, hivyo hawatawazuia wale
watakaotaka kuondoka Yanga.
"Ni kweli kabisa kanuni na
sheria za Fifa zipo wazi kuwaruhusu wachezaji waliobakiza miezi sita kufanya
mazungumzo na klabu nyingine, lakini tunatoa nafasi kwa wale wachezaji ambao
mikataba yao imemalizika watakaotaka kuondoka Yanga kwenda kufuata maslahi
mazuri.
"Ni ngumu kumzuia mchezaji
aliyeona maslahi mazuri kwingine, hivyo basi tutamruhusu kuondoka kama
unavyojua wachezaji soka ndiyo ajira yao, hivyo hatutaweza kuwazuia kuondoka
Yanga.
"Nimepata taarifa mbalimbali
za wachezaji wetu kuondoka mara baada ya mikataba yao kumalizika mwishoni mwa
msimu huu wa ligi kuu nami nabariki hilo," alisema Sanga.
Post a Comment