KOCHA ambaye anawaniwa kwa udi na uvumba na Yanga, George Lwandamina
ameamua kujiuzulu kuifundisha Zesco United na baada ya kuwaandikia barua mabosi
wake ambao pia wamekubaliana naye.
Lwandamina ambaye aliikisha Zesco hatua ya nusu fainali
kwenye Klabu Bingwa Afrika mwaka huu anatarajiwa kutua Yanga na kusaini mkataba
muda wowote kuanzia sasa.
Barua kutoka Zesco iliyotolewa kwa vyombo vya habari
inasema;
ZESCO United Football club inapenda kuwataarifu kuwa kocha
Mkuu George Lwandamina amejiuzuru asubuhi ya leo.
Klabu imekubaliana naye, tunapenda kumshukuru kwa kazi yake
na mchango wake kwa klabu yake akiwa hapa.
Lwandamina alijiunga na Zesco mwaka 2014 ameshinda ubingwa
wa ligi mara mbili mfululizo, kombe moja la Barclays , Ngao Ya Jamii na
ameiongoza klabu kufika nusu fainali ya klabu bingwa barani Afrika mwaka 2016.
Klabu inamtangaza kocha msaidizi Tenant Chembo kuwa kaimu
kocha Mkuu mpaka kumalizika kwa msimu huu.
Tunamtakia kila heri na mafanikio Lwandamina katika safari
yake mpya.
Imetolewa na
Justin Mumba na Katebe Chengo
Mkurugenzi mtendaji wa klabu na Afisa habari
Post a Comment