KOCHA mpya wa
Yanga, George Lwandamina tayari anawajua baadhi ya wachezaji wa Yanga ambao
anaamini wanamfaa katika kikosi chake.
Katika mechi moja
tu aliyokuwa ameiona awali wakati Yanga ikiivaa JKT Ruvu ikiwa ni ya mwisho ya
mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara, amesema yule rasta, yaani Thabani
Kamusoko, yuko sawa kabisa.
Awali, Lwandamina
alisema hawezi kuacha wachezaji kama ambavyo imekuwa ikiripotiwa, badala yake
angependa kuona zaidi DVD kadhaa za mechi za Yanga.
Lakini kuhusiana
na Kamusoko alisema anaona ni mchezaji ambaye anaweza kukidhi hata mahitaji
yake katika safu ya ulinzi kwa maana ya kiungo mkabaji.
“Nilimuona
akicheza na anajua nini maana ya kiungo mkabaji, anafanya nini na kipi
kinatakiwa. Ni mchezaji mzuri,” alisema.
Baada ya kuuliza
anatokea wapi na akaelezwa, Lwandamina akasema:
“Ok, kumbe ni
mgeni. Lakini amenifurahisha na mwingine ni yule alicheza kiungo cha juu, yaani
namba nane (ni Haruna Niyonzima),” alisema.
Alipoelezwa kuwa
ni raia wa Rwanda na kutajiwa jina lake. Cha kwanza alisema:
“Jina lake la
pili linanishinda, ni refu sana. Lakini ni kiungo mzuri sana ambaye atakuwa na
msaada.”
“Lakini suala la kusema
namuacha nani, namchukua nani, bado linahitaji muda. Vizuri nikiwaona
wachezaji,” alisisitiza.
Kocha huyo pamoja
na kufika jijini Dar es Salaam muda mrefu ameendelea kubaki mafichoni katika
hoteli moja ya kisasa jijini Dar es Salaam ikionekana uongozi wa Yanga unataka kumaliza
kila kitu kabla ya kumtambulisha.
Post a Comment