BEKI wa kati wa Yanga, Pato Ngonyani, amesema kama kocha
mkuu wa kikosi hicho, Mholanzi Hans van der Pluijm, angempa nafasi ya kucheza
mara kwa mara sasa hivi angekuwa kwenye levo nyingine.
Beki huyo alionyesha uwezo mkubwa katika mpambano wa watani
wa jadi Simba msimu uliopita akicheza kama kiungo, mchezo ambao ulimalizika kwa
Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Mchezo huo ulikuwa wa kwanza kwa Pato kucheza timu hizo
mahasimu zilipokutana ambapo uwezo aliuonyesha uliwakosha mashabiki na sasa
anadai kuwa kama angeendelea kuaminiwa na kupewa nafasi angekuwa mhimili mkubwa
kwenye kikosi hicho.
Pato alisema kama kocha wake akimpa nafasi kwenye mchezo
wowote ataonyesha uwezo mkubwa kwani licha ya kwamba kuna idadi kubwa ya
wachezaji katika kikosi chao hicho anaamini yeye ni mpambanaji.
“Mimi naamini kwamba ninacho kiwango kizuri na kama kocha akinipa
nafasi katika mchezo wowote nitacheza kwa juhudi zangu zote ili kuwaaminisha
hiki ambacho ninakisema,” alisema Pato.
Pato ni moja ya mabeki ambao wanatarajiwa kuziba nafasi za
akina Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ambao umri unawatupa mkono na muda wowote wanaweza
kutundika daluga.
Post a Comment