MSHAMBULIAJI hatari wa Yanga, Donald Ngoma pamoja na beki kisiki, Vincent Bossou, huenda wakatimka Yanga kama mipango yao itakwenda vizuri.

Taarifa ambazo tuezinasa zinadai kuwa Ngoma, ambaye amekuwa akiwindwa kwa muda mrefu na Mamelodi Sundown ya nchini Afrika Kusini, kuna timu moja nchini Urusi imevutiwa naye.

Taarifa hizo zinadai kuwa, timu hiyo ambayo inashiriki ligi daraja la juu, imevutiwa naye baada ya kumuona akifanya kazi kubwa Yanga ilipokuwa ikishiriki michuano ya kimataifa na huenda akatimkia huko.

Mbali na timu hiyo, taarifa nyingine zinadai kuwa, hata Mamelodi nao bado hawajakata tamaa ya kumfukuzia saini yake, huku pia baadhi ya timu nyingine nchini humo zikitajwa kumtaka.


Kwa upande wake Bossou, ambaye ni beki tegemeo kwa Wanajangwani hao, taarifa zinadai kuwa kuna timu moja kubwa nchini Ufaransa inamtaka, ambapo kama mambo yakiwa mazuri, naye atatoa mkono wa kwaheri.

Bossou, ambaye alianza kuitumikia Yanga kwa kusuasua na usajili wake kutajwa kama moja ya sajili mbovu, alikuja kuzinduka na kuonyesha uwezo mkubwa na kuwa tegemeo na sasa anatafutwa kila kona.

Post a Comment

 
Top