TAARIFA
zilizozogaa mitandaoni zinadai kuwa wachezaji wa Mbeye City wameingia uwanjani
leo kwa kuruka ukuta katika uwanja wa Sokoine, Mbeya wakijiandaa kucheza na
Yanga, lakini habari za uhakika zinasema tukio hilo sio la kweli na watu
wamekuwa wakieneza uongo huo ili wenyeji hao wahusishwe na imani za
kishirikina.
Mbeya City
na Yanga zinakutana leo kwenye Uwanja wa Sokoine mjini hapa, katika mchezo wa
ligi kuu ambao unaonekana kuvutia watu wengi kutokana na ushindani uliopo hivi
sasa.
Mwandishi wetu
aliye mkoani Mbeya amesema, wachezaji wa Mbeya City hawajaruka ukuta isipokuwa
uwanjani hapo kuna mageti mengi ya kuingia hivyo wao walipita kwenye geti dogo
ambalo basi haliwezi kupita eneo hilo hivyo kulazimika kuwashusha wachezaji na
lenyewe kuzungumza hadi kwenye geti kuu.
“Hizo
taarifa za kwamba wachezaji wameruka ukuta siyo za kweli kwani wachezaji
wamepota kwenye geti dogo ambalo gari haliwezi kupita na huwa halitumiki mara
kwa mara, kilichofanyika ni kwamba baada ya basi lao kufika liliwashusha
wachezaji na lenyewe kwenda kuingilia geti kubwa,” alisema mwandishi wetu.
Aidha Yanga
pia walitinga uwanjani hapo wakiwa na basi dogo la kukodi na walipoingia tu
walipokelewa kwa shangwe kali na mashabiki wao.
Post a Comment