HIVI karibuni kiungo mkabaji wa Simba, Jonas Mkude ambaye
mkataba wake na timu hiyo unafikia tamati mwezi Januari mwakani, alisema kuwa
mpaka sasa haelewi chochote kama ataendelea kuitumikia timu hiyo au la.
Kutokana na hali hiyo, Mkude akawataka Yanga wakamsajili
kama kweli wanamhitaji akidai bila kusita atasaini timu hiyo, kwani yupo tayari
kuitumikia.
Jambo hilo linadaiwa kuukera uongozi wa Simba na umeamua
kuchukua jukumu la kukaa kimya bila ya kumfuatilia tena kiungo huyo na wamesema
kama anataka kwenda Yanga aende.
“Mkude hivi sasa anatakiwa kuwa makini sana, vinginevyo
anaweza kujikuta katika wakati mgumu kwani uongozi umesema kuwa hautahangaika
naye tena, yeye kama anataka kuondoka basi aondoke zake.
“Wamefikia hatua hiyo baada ya kumbembeleza sana kusaini
mkataba mpya lakini yeye amekuwa akizingua akidai kuwa fedha anazotaka kupewa
ni kidogo lakini pia kila akiitwa kwa ajili ya mazungumzo amekuwa akikataa,”
kilisema chanzo chetu cha habari na kuongeza:
“Kutokana na hali hiyo uongozi wa timu unamsubiria kocha aje
ili uweze kuzungumza naye na ikiwezekana aanze kuwa anamtumia Mzamiru Yassin
kama kiungo mkabaji halafu Juma Awadh awe anacheza namba nane.”
Alipotafutwa Mkude ili aweze kuzungumzia hali hiyo alisema:
“Kama wamefikia uamuzi huo ni wao lakini binafsi kwa sasa siwezi kusema
chochote juu ya suala hilo.”
Post a Comment