MABINGWA
watetezi wa Ligi Kuu Bara, Yanga leo wameumaliza kwa furaha mzunguko wa kwanza
wa ligi hiyo baada ya kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ruvu Shooting katika
Uwanja wa Uhuru jijini Dar.
Yanga
iliingia uwanjani ikiwa inajiamini kuwa itaondoka na alama tatu dhidi ya
maafande hao lakini walijikuta wakipigwa bao la kushtukizwa dakika ya saba
kupitia kwa Abdulhaman Mussa ambaye alitumia uwezo binafsi na kupiga shuti
ndani ya 18 lililomuacha kipa Beno Kakolanya wa Yanga akijaribu kuudaka bila
mafanikio.
Baada ya bao
hilo kuingia, Yanga walikuja juu kutaka kusawazisha kitendo kilichowafanya wachezaji
wa Ruvu wote kurudi nyuma kuzuia mashambulizi ya wapinzani wao hao.
Dakika ya 31
Haruna Niyonzima alitengeneza nafasi nzuri iliyotokana na kumpiga chenga ya
kimaajabu mlinzi wa Ruvu kabla ya kupiga krosi nyepesi kwa Msuva ambaye
aliukwamisha wavuni mpira na huo hivyo kupelekea timu hizo kwenda mapumziko
wakiwa sare ya bao 1-1.
Kipindi cha
pili Kocha wa Yanga, Hans Pluijm aliondolewa kwenye benchi lake na kutakiwa
kukaa jukwaani baada ya kuonekana akizozana na mwamuzi. Hali hiyo haikuonekana
kuwakatisha tamaa kwani walipambana na kufanikiwa kuanidka bao la pili dakika
ya 56 mfungaji akiwa ni Niyonzima.
Ilikuwa
hivi; Donald Ngoma alipigiwa mpira mrefu karibu na lango la Ruvu kisha
akajaribu kupata kufungwa lakini mpira ukambabatiza kipa wa Ruvu kabla ya Ngoma
kuuwahi akiwa amekaa chini na kumpasia Niyonzima akiwa nje ya 18 ambapo alichia
shuti kali lililojaa wavuni.
Baada ya bao
hilo kuingia, Ruvu walionekana kuja juu kutafuta bao la kusawazisha na kisha
kuongeza la ushindi lakini washambuliaji wake walionekana kutokuwa makini hasa
walipokuwa ndani na nje ya 18 kwa kupiga mpira nje au kuokolewa na mabeki na
kipa wa Yanga.
Post a Comment