London, England
WIKIENDI iliyopita pale Old Traford
tulishuhudia mtanange mkali kati ya wenyeji Manchester United ambao walibanwa
na Arsenal na kutoka nayo sare ya bao 1-1.
Mchezo huo uliokuwa wa raundi ya 12
ulishuhudiwa Man United wakiwa wa kwanza kaundika bao lao kupitia kwa Juan Mata
kabla ya ‘super sub’ Giroud kuisawazishia Arsenal dakika za mwishoni.
Leo ninakuletea nyota watano ambao
wamewahi kucheza Man U halafu wakatimkia Arsenal au kinyume.
5) Mikael Silvestre
Mashabiki wa Arsenal hawataki kabisa
kulisikia jina la mchezaji huyu. Jawakuvutiwa kabisa na usajili huu, ilionekana
kama Arsene Wenger alikurupuka kufanya usajili wa Silvestre.
Beki huyo ambaye ni Mfaransa, akiwa
United alicheza misimu tisa na kufanikiwa kutwaa makombe matano ya ligi, FA Cup
na Champions League. Alicheza mechi 249 chini ya Kocha Alex Ferguson ambaye
alimsajili kutoka Inter Milan mwaka 1999.
Kwa muda mrefu alikuwa akicheza kikosi
cha kwanza kabla ya kuibuka kwa nyota Rio Ferdinand, Nemanja Vidic na Patrice
Evra ambao walimuweka benchi.
Wenger alimsajili mwaka 2008 akiwa
hayupo kwenye kiwango chake kutokana na kutocheza kwa muda mrefu. Akiwa hapo
alikuwa akifanya makosa ya mara kwa mara uwanjani na alifanikiwa kucheza mechi
26 katika misimu miwili kabla ya kutimkia Werder Bremen.
Frank Stapleton alikuwa ni mmoja kati
ya washambuliaji bora pale Arsenal lakini pia alifanya vyema akiwa Man United. Huyu
bwana alienda kufanya majaribio Arsenal na Man United lakini mwisho wa siku
akagomea ofa ya United na kutua Gunners. http://spotiripota.blogspot.com/
Alicheza jumla ya mechi 225 na
akafanikiwa kuibuka mfungaji bora katika msimu mitatu mfululizo. Alifanikiwa
kucheza fainali tatu za Kombe la FA lakini akabeba moja ambapo kwenye ushindi
huo alifunga bao la tatu ambalo lilikuwa la ushindi (walishinda 3-2) dhidi ya
United.
Hata hivyo iliripotiwa kuwa nyota huyo
hakuwa na furaha zaidi kutokana na kutopata mafanikio akiwa kikosini hapo hivyo
akafanya maamuzi magumu. http://spotiripota.blogspot.com/
Aliachana na Gunner na kutimkia United
mwaka 1981 ambapo hapo alifanikiwa kucheza mechi 223. Alifanikwa kuchukua
makombe mawili ya Kombe la FA mwaka 1983 na 1985.
Anarekodi ya kufunga bao akiwa na
klabu mbili na kila moja kuifungia bao kwenye mchezo wa fainali wa Kombe la FA.
3) Geroge Graham
Haina ubishi kuwa Graham anabaki kuwa
mmoja kati ya malejendi pale Arsenal na hiyo ni kutokana na mashabiki wengi
kuonekana kumkubali kutokana na mafanikio aliyoyapata sio tu akiwa mchezaji
bali hata alivyokuwa kocha, lakini pia aingia kwenye rekodi ya kuwa kati ya
nyota wachache waliowahi kucheza Chelsea, United na Arsenal.
Graham aliondoka Arsenal mwaka 1971 na
kujiunga Man U mwaka uliofuata na akiwa hapo akacheza kwa msimu mitatu. http://spotiripota.blogspot.com/
2) Viv Anderson
Huyu naye alikuwa mmoja kati ya nyota
waliocheza katika timu hizi kwa nyakati tofauti. Lakini pia kama hujui huyu
ndiye mchezaji wa kwanza mweusi kucheza timu ya Taifa ya England ambapo jumla
alicheza mechi 30. http://spotiripota.blogspot.com/
1)
Robin Van Persie
Huyu jamaa aliondoka Arsenal na
kujiunga na Man U mwaka 2012 na kutengeneza chuki nzito kati yake na mashabiki
wa Arsenal.
Robin Van Persie, ambaye alikuwa
mfungaji bora kikosini humo kabla ya kuondoka ambapo ndoto zake kubwa zilikuwa
ni kutafuta kombe hivyo akaona sehemu ambayo atalipata kabla ya kustaafu ni
United na kweli alipotua msimu huohuo akalipata.
Hata hivyo nyota huyo alidumu kwa
miaka miwili tu klabuni hapo kabla ya kutimka. http://spotiripota.blogspot.com/
http://spotiripota.blogspot.com/
Post a Comment