WAAMUZI wamesema hawatachezesha mechi za Simba endapo ombi la timu hiyo la kutaka waamuzi wa mechi yao na Yanga watoke nje ya nchi litapitishwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Simba kupitia Ofisa habari wake, Haji Manara mapema wiki ilitoa tamko la kugomea mechi zake dhidi ya Yanga ikitaka zichezeshwe na waamuzi kutoka nje ya nchi wakihisi kuhujumiwa na wale wa ndani.
Baada ya kauli hiyo, Mwenyekiti wa Chama cha Waamuzi Tanzania (Frat), Nassoro Mwalimu, kwanza amelaani kauli hiyo ya Simba pia akasema wakikubaliwa basi wao watagomea mechi zote za timu hiyo.
“Kama wanataka kushinda mechi zao kirahisi, basi waombe na mechi zao zikachezwe Uwanja wa Wembley (uliopo London, England) ili washinde kama wanavyotaka.
“Wametutukana sana na wanatakiwa watuombe radhi, huku ni kudhalilisha waamuzi na taaluma yenyewe, wanatakiwa watueleze upungufu wetu na si kutudhalilisha kiasi hiki.”
“Wasituangushie lawama sisi waamuzi kitu ambacho hatukubali tukiona tunapewa mzigo huo wa lawama, niwaulize tu, walivyomfunga Yanga mabao 5-0 walichezeshwa na waamuzi kutoka wapi?

Post a Comment

 
Top